03 January 2011

Abramovich atumia bilioni 11 kusherehekea mwaka mpya

LONDON, Uingereza

WAKATI watu wengi wakifikiria watapataje fedha, lakini wengine kwa hilo si tatizo, kwao tatizo ni jinsi ya kutumia.Tajiri wa Kirusi, ambaye ni mmiliki wa timu ya ya soka ya Chelsea, Roman Abramovich,  aliamua kutumia fedha
kufurahi yeye pamoja na watu wengine maarufu aliowaalika katika sherehe ya kuuanga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2011.

Sherehe hiyo iliyofanyika katika kisiwa vya St. Barts Carribbean,  inaelezwa kuwa, ilikuwa ya kufana pengine ni sherehe nzuri zaidi kuliko zote, ambapo miongoni mwa wageni waalikwa, walikuwa ni wasanii maarufu wa Jiji la Hollywood, Marekani na bendi maarufu ambazo ziliburudisha wageni waalikwa.

Tajiri Abramovich, alionekana kama kuwa mtu wa kawaida na kujichanganya na watu wengine kucheza.

Sherehe hiyo ya mwaka mpya ilimgharimu pauni milioni 5 ambazo ni sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya sh. bilioni 11.

Pamoja na kuwepo wasanii maarufu kama marapa wa bendi ya Black Eyed Peas, bilionea wa  Russia alionekana kama ni wa kawaida tu, hakupagawa kwa furaha kama walivyokuwa watu wengine.

Abramovich alionekana kama ameboreka, lakini kulikuwa na mastaa kama Salma Hayek na Demi Moore.

Wageni waalikwa katika sherehe hizo walikuwa wamevalia mavazi ya bei mbaya, akiwemo mwanamitindo aliyegeuka kuwa, mwigizaji wa Uingereza, Rosie Huntington.

Lakini, mmiliki huyo wa  Chelsea, alionekana kuwa katika hali ya utulivu, akiwa karibu na mkewe Daria Zuchova, kwa kuandaa sherehe hiyo iliyomwongezea umaarufu wake.

Mwaka 2009, alitumia pauni milioni 3, zaidi ya shilingi bilioni 6.6, kwa sherehe kama hizo za mwaka mpya, ambapo nyota kama Orlando Bloom na Kanye West walitumbuiza na Prince, Gwen Stefani na Beyonce.Abramovich inaaminika alimlipa Prince pauni 500,000, ambazo ni zaidi ya sh.bilioni 1.1.Haikujulikana mara moja kwamba, kundi la Black Eyed Peas lililipwa kiasi gani, bila shaka itakuwa ni fedha nyingi.

 Abramovich mwenye miaka 44 na mkewe Zuchova mwenye miaka 29, ndiyo waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye geti katika eneo lake alilonunua kwa pauni milioni 58, lenye ukubwa wa ekari 70, liliko karibu na Governor Beach katika kisiwa cha Caribbean.Eneo hilo lenye nyumba, mabwawa ya kuongelea na vitu vingine liko bahari, awali lilikuwa likimilikiwa na familia inayomiliki benki Marekani ya Rockefellers.

Baadhi ya wageni waliokuwepo ni panmoja na mwelekezaji wa filamu ya Star Wars, George Lucas, rapa Sean P.Diddy Combs, Ellen DeGeneres, mwimbaji Alicia Keys na Harvey Weinstein, walipelekwa katika kisiwa cha St Barts kwa helikopta kabla ya mwaka mpya.

Katika sherehe hiyo, inaaminika kuwa, Abramovich alitumia mamilioni kwa ajili ya kununua chakula na vinywaji vya wageni 2,560, aliowaalika.

Katika ufukwe kulikuwa na boti yake ya kifahari ambayo inatajwa kuwa ni ndefu kuliko zote duniani, pia ilikuwepo boti ya bilionea mwingine wa Kirusi Andrey Melnichenko, ambayo ina vyumba vya kulala, rasmi kwa wageni ambao walikuwa hawataki kulala kwenye nyumba zilizopo kwenye uzio.

Mwaka mpya wa 2011 ulipowadia, fataki zililipuliwa kutoka kwenye boti na kuwafanya wageni wafurahie. Siku moja kabla ya mwaka mpya, Roman na Daria, mama wa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja Aaron, walionekana wakienda kwenye boti yake ya kifahari yanye urefu wa futi 543.

Boti hiyo yenye thamani ya pauni milioni 300, ina vyumba 12 na walinzi watano na sehemu ya kuangalia sinema, maktaba na mgahawa. Pia, inaelezewa kuwa, imetengenezwa katika mfumu  ambao paparazzi hawawezi kupiga picha ikiwa pia haiwezi kulipuliwa.

No comments:

Post a Comment