Uchumi na Biashara

Wakulima wa vitunguu Singida wapata bil. 3.5/-
 
Na Thomas Kiani,Singida

WAKULIMA wa vitunguu mkoani Singida msimu uliopita walizalisha tani 17,334 za  vitunguu zenye thamani ya sh.bilioni 3.5 katika maeneo yanayolima zao hilo kwa wingi na kuuzwa kwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.
 
Taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Kilimo Mkoa wa Singida, Bw.Deusdedit Rugangila zilieleza  kuwa
wafanyabiashara kutoka Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, India na Comoro na wengine kutoka Mikoa ya Manyara, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ndiyo wanaoongoza kununua vitunguu vya Singida kwa wingi katika soko lililotengwa.
 
Bw. Rugangila aliyataja, maeneo yanayolima vitunguu kwa wingi Wilaya ya Iramba kuwa ni Mwanga, Nduguti, Gumanga, Ilunda na maeneo mengine ni Iguguno, Ulemo, Msingi, Singa.Maeneo yanayolima vitunguu wilayani Singida ni Mtinko, Merya, Kinyeto, Ilongero, Ikhanoda na mengine ni Mdida, Mwanyonye, Msange na Ngamu. 

Ilieleza  wakulima wa vitunguu huanza kutayarisha mashamba yao mwezi Novemba hadi mwezi Aprili, tayari vitunguu huanza kuvunwa na kuuzwa


Bw. Rugangila alitaja mbegu za vitunguu zinazolimwa sana Singida kuwa ni Red Bombay, Red Globe, Red Creole na Tropicana na amewahimiza wakulima kutumia mbegu bora ili waweze kupata mazao mengi na bei nzuri ili kukidhi mahitaji ya soko. 


Hata hivyo amewahimiza wakulima kutumia mashamba darasa yaliyopo kwenye maeneo yao ili waweze kufikia malengo yanayotakiwa.
 
Mkoa wa Singida katika miaka ya nyuma ulikuwa maarufu sana kwa uzalishaji wa vitunguu lakini sasa uzalishaji wake umeanza kupungua kutokana na uhaba wa mvua,kukosa dawa za kuua wadudu, ukungu na utaalamu mdogo juu ya upandaji, uvunaji na utunzaji wake.
 
 

Amana yazindua huduma zake Dar
Makumba Mwenezi na Mariam Bokero

WATANZANIA wameanza kunufaika na huduma za kibenki zinazofuata misingi ya dini ya Kiislamu baada ya kuzinduliwa rasmi kwa benki ya 'Amana'ambayo itaendeshwa kwa kufuata misingi ya sharia na maelekezo ya ufanyaji biashara ndani ya Quran tukufu.

Benki hiyo ambayo ni benki ya kwanza ya Kiislamu Tanzania ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuanza kutoa huduma siku hiyo hiyo, huku ikiwa tayari imetoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 50 katika nafasi mbalimbali.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa benki hiyo, Mwenyekiti wa bodi, Bw. Haroon Pirmohamed alisema Amana benki itatoa huduma na bidhaa ambazo zitafuata misingi ya sharia na ambazo zimepitiwa na Bodi ya Sharia kwa mujibu wa Quran.

Alisema huduma hizo ni pamoja na akaunti za biashara zisizokuwa na riba yoyote, akaunti za akiba, akaunti maalumu za wanawake na watoto, akaunti za hijja na akaunti za akiba kwa ajili ya nyumba za ibada zilizosajiliwa yaani Ihsan akaunti.

Bw. Permohamed alisema benki imedhamiria kutoa huduma katika mazingira rafiki kwa wateja hasa wale wote wasiofurahishwa na huduma za riba zinazotolewa na benki nyingine na kudai kuwa huduma za benki hiyo ni kwaajili ya watu wote wakiwemo Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Amana benki inatokana na michango ya mjumuiko wa wafanyabiashara wanao amini na kufuata misingi ya sharia kikamilifu na inamilikiwa na Watanzania wazalendo wakimiliki hisa tofauti huku benki ikiwa na kiasi cha mtaji wa sh. bilioni 21.1 mpaka sasa.

29 comments:

  1. Tatizo la bank ya crdb inayojitangaza mkombozi wa maisha ya mtanzania ni waongo sana.moja riba wanayocharge utazania ni mjerumani anayekopa kumbe ni huyo mtanzabnia wa kipato cha chini ya dol moja kwa siku.kupata huo mkopo utadhania hata kama ulikuwa na biashara mpaka ipite ndiyo upate huo mkopo.na ukiomba milion moja mfanao utapewa laki nne ili tuu ushindwe kulipia kile ulichokuwa uantarajia./kwa hiyo hapo waseje kudanganya watanzania kwamba hiyo ni bamnk ya walalahoi wakati riba ni kubwa kuliko bank zingine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Open Letter From Valerian Family!
      Dear all in the name of Jesus our Lord and savior.

      I have been keeping quiet for some times, but Jesus calls us all to use our intuitions and speak out the truth and only the Jesus kind of truth that he died on the cross for. I'm Valerian Family member and I had the greatest opportunity to talk to him every other Sunday, and I saw him in his last days fading away. It was the hardest thing to see a fellow human being going through. Only Lord God Jehovah can understand the pain and anguish of his passing, yet the kind of things this young family is going through, sadly from the very people who are suppose to guide and protect this young family.

      The history is as bad to the point that Some Balthazar Family members got so hateful and jealous to ask publicly "Why there is no death in the Valerian's Family? OR "why none of the Valerian's children are dying like ours?". This is kind of things that growing to this level can lead such hatred to deceive people and take matters on their hands to cause death, as they wish it so bad. But what they dont understand, there is God and that the widow, Mama Pendo, was a nurse first before she became a teacher, who could health identify problems of her kids at very early stage and seek medical treatments. While some family members, possibly, were going for traditional medicine and possibly let sickness grow on to their children beyond repair. But when faith is involved you cannot just fade it away as simple as i explained above, or just wipe out the decades of hatred. We need help and that help is from the institution like yours. More payers and God given guidelines. We need it desperately.

      We have a problem. It is problem rooted in the Chagga People Tradition of invading widows' home and oust them and their children to fend for themselves after the father, head of the family as God divinely granted them, passes away. This is done without remorse and no one, even the most educated and or exposed to the Western Civilization Culture life style are doing it and or witnessing it in their own families and don't say or do a thing about it, in spite of their knowledge that is not the right thing to do. It is bothering because I know my mother in-law and I know Auntie Florentina Masawe and Bernadin Marselian Masaawe and I have see and studied their moves. There is an issue of Uru People against Women from Marangu and married in Uru. It is hateful and dangerous and need your and our attention all
      This instrument of spreading the word of God can be used wisely and justly to become an agent of change and change that is needed now. Unfortunately, the laws are so vague and have so much gray area that the devil is using them to advance the oppression against widows and the vulnerable.

      You see, God gave us everything to better our relationship with him, but the devil as master minder, manipulator in chief, lair, master musician, master negotiator and destroyer, uses the same world we were given by God through the free-will, including laws and traditions, to destroy us. That is the truth and that is the Jesus Kind Of Truth that Jesus was Crucified for on the Cross and ultimately die for, so we can be salivated. Understanding the truth and the world that we are living is the key path to God in Heaven.

      Please, visit this Link here and evaluate all the facts by yourself and see how God sent you to help in this. We need prayers because this is the spiritual warfare that need prayers than just laws, rules and regulations. The devil is riding up in here hard and we need all the prayers we can get. http://florentinamasaweinvadesvalerianhome.blogspot.com/

      God is great and keep on the good job of God. A we say Amen!!!!!!!!!!!!!


      Hope, on Behalf of Valerian Family.

      Delete
  2. JAMANI SASA MAMBO NI MSHIKEMSHIKE HAPA ARUSHA.
    NAOMBENI MUONGOZO WENU KIDOGO,HUYU MDUDU ANAYEITWA PAD AMEZALIWA NCHI GANI HUKU DUNIANI?ETI KUNA MITHALI INAYOSEMA KUFA KAFAANA,LAKIN HII YA SASA NI KUFA NA UMALIZIKE KABISA.
    MIMI NI MFANYABIASHARA NDOGO KABISA WA DUKA,LAKINI NINAAGIZA MALI KIDOGO TUU KUTOKA NCHI JIRANI YA KENYA ,UGANDA,UWEZI KUAMINI UNAKAA MPAKANI MWA NAMANGA ZAIDI YA SIKU 21 MPAKA 30 ETI UNANGOJA KUPEWA IDHINI NA WATU WANAOJIITA OQS WALIOKO NCHI INAYOITWA DSM.MIMI NINADAIWA NA BANK NA NINATAKIWA KURUDISHA MAREJESHO YA BANK KILA MWEZI,LAKINI LORR LINAKAA MUDA WA MWEZI MZIMA KWENYE MPAKA WA NAMANGA LIKISUBIRI HUYO MDUDU ANAYEITWA PAD.ZAIDI KABISA UNAAMBIWA USIPOTOA ELFU HAMSINI YA KUSUKUMA PAD UNAWEZA KUKAA ZAIDI YA MUDA HUO NILIOUTAJA.BADO LORR TUNALIPIA KILA SIKU LINAPOKAA MPAKANI JUMLA YA TSH (150,000)YAANI USD 100 KWA KUCHELEWESHA LORRY LA WENYEWE,JE UO NDIO KUTUKOMBOA KWENYE UMASKINI WA WANYONGE NCHI HII AU NI KUTUMALIZA KIBIASHARA 8ILI WALE WAKUBWA WAZIDI KUTUFANYA MANAMBA WAO MPAKA KIHAMA.NAOMBENI MNISAIDIE KUPATA MAJIBU HAYA ILI NIJUE KAMA MIMI NI MWANANCHI AU NI MKIMBIZI NCHINI KWANGU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani wasenge sana kaka. That is not the way to do business at all brother! The leaders and the right wings are all not educated well about leading a country. They forget about the importance. Police, na wahusika wote wasenge. Nichagueni mimi to lead the country that we lost since our indepence. Matatizo kama haya, yanawafanya watu kama wa Zanzibar kujitoa kabisa. I'm not mad at them at all brother! More power to them. The importance thing that we need to do as Tanzanian, we need to form a union to make it as a company. That is the only way to protect our businesses. Otherwise, you will still be treated as a second class citizen in your own country and the muhindi will be first class. Do you want that? You see that happening everyday. Mimi nafikiri sisi tuna uswahili mwingi sana na tunakosea kutoungana kutengeneza umoja wa Taifa. Angalia mataifa mengine, wao huunda union to protect there interest. This will also protect the next generation. Police akimuona muhindi au mzungu, wanatetemekea dolla. Huo ni usenge sana wa kusahau watu wao. I'm very sory to here that brother. Kwa sasa mimi niko US na ninasikia kwamba kampuni kubwa zitakuja huko kununu alithi nyingi. Tusipo jiangalia kimakini, wote tutakimbilia mjini baada ya kukaa shambani na kutengeneza pesa ya maana. Mzungu na muhindi atanufaika na shamba lako kwa faida kubwa wakati ukipiga mwayo.

      Delete
    2. Kaka nimekusoma! Lakini unaposema tuanzishe something that me and you may call it as 'taasisi ya wananchi wa Tanzania'ni sawa! lakini ni nani atakisajili kwa sababu nionavyo matatizo ya nchi yalishaonekana from when the nation was created. I believe that Tz tumegawanyika sana na tatizo lipo na linaonekana na watu wa nchi hiyo ambao ni watazania wanalijua! but wametenganishwa na kitu kimoja! the elites have made it clear that most of national resources such as madini, gesi, mashamba mazuri has yale ya ranchi za taifa will never be re-invented to wananchi kwani kufanya hivyo wataelimika and develop a strong collective forces. In addition, rural education is likely being unavailable. Shule za kata ndo hizo babu yangu hakuna kitu pale mie naona wazifunge na hayo majengo wapangishe kama magodown watu akodishe waweze kuhifadhi mazao or something. nikiwa na maana kwamba hizo shule hazina maabara, inadequate building structures and no waalimu wenye enough profession au hata resources za kufanya research kama vile computers na hata kama zipo umeme au gharama zitatoka wapi wapi wakati waziri wa fedha ana taka kuongeza kodi kwenye 'soda' wakati elites wakitanua na kodi zetu kwenye madini jamani?????

      Correct me when i am wrong guys...

      Delete
  3. Inasikitisha sana kuona jinsi watendaji wetu wa kazi serikalini ktk ngazi zote kuanzia wafagizi mpaka maafisa walivyo warasimu. Upande wangu ninaona nivema kuunda vyombo au umoja wa wafanya biashara za nje ya nchi ili kiweze kukusanya malalamiko yao yote kupeleka serikalini na kama tatizo halisikilizwi basi moja kwa moja hadi kwa rais ili ajue shida gani mnapata. Kitu cha kufurahia ni kwamba sasa hivi technology imekua kiasi ambacho watu wengi wana simu zeney Camera na recorders ambazo zinaweza kusaidia kufichua ubadhilifu wa hao wafanyakazi wa serikalai wanaorudisha nyuma gurudumu la maendeleo.

    ReplyDelete
  4. Jamani habari zamchana nasikitika wito wangu ni kukubali kuwa watanzania tumefika mahali pa kutokudhaminika hata kama unalipa hiyo kodi,tumekuwa kama wapanda daladala maana daladala mteja kwao ni yule hajapanda na kulipa nauli ukishalipa basi wewe una dhamani tena,hata ukikanyagwa na kuvunjika mguu hiyo kwa wakati huo hawana shida tena umeshawalipa pesa yao.ndiyo kama vile tra sasa,umeteseka kuenda kununua mali yako umeshaweka pesa kwenye tembo kadi yao,ina maana pesa yako na mali yako wanayo,cha kushangaza wanaweka lorr siku 21-30 mpakani huo si unyama kabisa wenzangu na mimi?au ndiyo wanaamua kutengeneza mazingira ya rushwa ili watu watafute njia mbadala ili wawe watumwa wa kubembeleza wafanyakazi wa tra wakati hatakapokutana naye wakati ajalipia huo mzigo wake?huyu bwana mkubwa anayeitwa mkulo,na huyu kitila wanaona ni sawa watanzania kuteswa hivyo?naomba hawa wakubwa waangalie jinsi watanzania wanavyoteswa na pesa yao mpaka kuwa maskini wa kutupwa,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawa viongozi wanajua sana. Huwezi kua kiongozi na usijue kitu gani kinachotendeka mpakani mwako. Mimi kinacho nishangaza nikwamba, kwanini watu wa kijiji au jiji hilo wasiandamane? Umoja nikitu cha muhimu sana. Trust me, the leaders know this. Yaani basi tu. Niwajinga. Not enough education to lead the country. Wao hujifikia wao tu na maisha yao. They forgot about the next generation. Wewe ushikilie gari kwa mwezi, hiyo ni maana gani? Nikama kuzuia uchumi kwa mwezi. These people need to be educated for real lol!

      Delete
  5. Naomba hii muiwekekwenye ukurasa wa mbele kabisa .

    WATUMISHI WAPYA KARAGWE WALALAMIKIA KUTESEKA
    Sisi watumishi wapya wa halmashauri ya wilaya ya karagwe tunateseka sana ,kwa kutopewa mishahara yetu kwa wakati na kingine kibaya zaidi pesa zetu za kusafirisha mizigo hatujalipwa mpaka sasa . Inaonesha kuwa uongozi haujali kabisa tabu zetu ,serikali bungeni inaongea tu kwamba watumishi wote wapya walipwe haki zao zote na imetoa maagizo kwa wakurugenzi husika wafanye hivyo lakini hamna kinachoendelea pesa zinakuja wanpanga mikakati ya kuhalalisha kuzila kwa safari na semina mbalimbali watumishi tunateseka . Hivi unadhani tutaipenda serikali yetu kihivyo ? unadhani watu watakuwa na morali ya kufanya kazi au kupiga kura kweli ? inasikitikisha sana . TUMECHOSHWA NA UONGOZI ULIOPO HAWATUTENDEI HAKI.

    Ni sisi watumishi wapya -Karagwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unda umoja wakujitetea jamani. Kwanini teseka? Sauti nyingi huleta vitendo. Bila sauti nyingi hamna atakae sikiliza. Epuka na ufisadi kwa kusema kitu kila unapoona ufisadi unatendeka. Barabarani, kazini, na sehemu zote. Viongozi walisha shindwa tangu Baba wa taifa alipo ondoka. Utapeli na kufilwa na wazungu pamoja na wahindi ni mwingi officini kwa sasa.

      Delete
  6. WATUMISHI WAPYA KARAGWE WALALAMIKIA UONGOZI KUTOWALIPA HAKI ZAO
    Sisi watumishi wapya wa halmashauri ya wilaya ya karagwe tunateseka sana ,kwa kutopewa mishahara yetu kwa wakati na kingine kibaya zaidi pesa zetu za kusafirisha mizigo hatujalipwa mpaka sasa . Inaonesha kuwa uongozi haujali kabisa tabu zetu ,serikali bungeni inaongea tu kwamba watumishi wote wapya walipwe haki zao zote na imetoa maagizo kwa wakurugenzi husika wafanye hivyo lakini hamna kinachoendelea pesa zinakuja wanpanga mikakati ya kuhalalisha kuzila kwa safari na semina mbalimbali watumishi tunateseka . Hivi unadhani tutaipenda serikali yetu kihivyo ? unadhani watu watakuwa na morali ya kufanya kazi au kupiga kura kweli ? inasikitikisha sana . TUMECHOSHWA NA UONGOZI ULIOPO HAWATUTENDEI HAKI.

    ReplyDelete
  7. Usilalamike PAD this is the results of what Mwl. was trying to build in this country for 40yrs. Put obstacles before any attempt to become entrepreneur so that kill capitalism now things have changed but the mind set of our people have not.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kulalamika = kupata haki. They have the right to do so. The main problem is our leader for failing to provide that education that could be able to wake everyone. Putting abstacles first before the rich of entrepreneurial is a comon sence. But, pointing out for what couses the obstacles and how to prevent it from happening again is the forcus. The mind of our people can only change after loosing everything. It didn't seem to change when people got to be sold in slaverly. Look at the leaders now, still doing poor jobs in waking up there onw people. Uswahili mwingi bila vitendo. What we see is the same thing. Ufisadi na umoja hamna. Wakifilwa na wazungu pamoja na wahindi oficini, hutufanya sisi tuwe second class sitizen in our own country. Maybe later we will learn after everything is gone and all the second class are Africans. Unity is awesome!!!!! Can kill all of that and you have a chance for the world to support you. Fuck the bulshit, form Union to protect our interest for the next generation to come!!!! Right now, the next generation don't have future. Maybe for the European and wahindi's kids. Definitely not for the Africans. How can you be fooled in your own country? Wake up Tanzanian!!!! Ubovu sisi ni wasenge wasenge sana. Tumekaakaa kama mademu pwani bana. Wake up na jitetee kama mwanaume!!

      Delete
    2. If the opposition parties unite and form a one front against CCM that may help and "chukua chako mapema" mind set/mentality has to dissolve and change from whomever is given power. Otherwise, may be REVOLUTION by young minds for the better of the nation. Mungu Ibariki Bongo na Watu wake!

      Delete
  8. Tatizo sisi watanzaniaa waogaaaaaaa!Tungekua sio waoga hawa watu wasingetuchezea hv. Angalieni wenzetu wa middle east walivyokua ngangari. by le grande

    ReplyDelete
  9. jamani hisa za SBL zikiuziwa TBL USHINDANI UTATOKA WAPI?FCC plz muwe makini.

    ReplyDelete
  10. Mambo ya biashara siyajui.
    Swali langu huyo mtu anayehusika na kuruhusu mizigo hapo namanga ni mtu timamu ??? samahani .
    Mizigo yote si mbao ,, je kama ni vitu vya kuoza ??
    poleni mnaoteseka. hakuna la kufanya zaidi ya kusalimiana hapa kwenye majira.(naitwa USIKANYAGE KWENU)

    ReplyDelete
  11. loh!kweli ndugu mfanya biashara kama hali ni hiyo kweli ni ngumu sana;lakini ni nani wakulaumiwa?uyo mdudu uliemtaja au selekali kwaujumla.kwasababu kama ubongo aufanyi kazi ipasavyo basi ujuwe mwiliwote ushakuwa kilema.kamaselekali yetu haina msimamo mzuri na ufatiliaji mzuri wa wafanyakazi mambo ndo kama hayo yaliyokukuta ndugu mfanya biashara.kazi ya kufanyika siku moja ukitaka kuifanya kialali itachukuwa miezi mitatu.ivi mnavyofikiri lushwa itaisha noo.na hiyo lushwa inasababishwa na selekali yenyewe kwautendaji wao mbovu wakazi.tuacheni kufimbia macho mambo kama haya mimi ningeomba hili gazeti letu la majira lioneshe kama linathamini haya maoni yetu.na kuyapigia debe hayo matatizo uliyoyaeleza ili wanachi wote waelewe hawe.kwani sasa jipu limeshaiva na nahisi kwampango huu wa serekali unaoendelea umeme,maji,mafuta,hakuna kazi vijana wanazungka mtaani,na halimbovu ya uchumi nduguzangu litapasuka mda simlefu mtaona damu tu. ni mimi mtanzania mwenzenu ninaitwa kijembe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kazi wanapewa watu wa nje wasio na kisomo na wala silazima waongee kiswahili. Mambo gani hayo? Ni kweli matatizo haya yanatokea selekalini. Maana wao huko hawajiwezi, na usitegemee wao kuweza matatizo yako na kuyamaliza. Kila siku ni longo longo za kiswahili. Mambo ya muhimu wala hayaongelewi sana. Pesa zikitolewa, za chai, soda, tumbo na mademu nazo lazima zitoke. Wewe unafikili tutaendelea hivyo. Raisi ananguvu za kubadirisha Taifa lake wakati wowote. Viongozi wa mitaani mpaka selekalini hawasimamiwi vizuri na kuhojiwa vitendo vyao. Ulushwa mtupu mpaka balazani. Wananchi watakiwa kutengeneza umoja. Unity will kill all of these nonsence. Form union for everything Tanzanian!!! Otherwise you will still continue to be stolen just like the slaverly time. Those events have naver changed since and i don't know if you realize that. Nchi bado inaibwa kila siku na wakati ndugu zako kijijini wazidi kuteseka na kufukuzwa kwenye mashamba yao. Hostoria, mira na desturi zinazidi kupotea kila siku. Basi wote tuwaige wazungu na tutupe zetu. Fundisha mtoto kiswahili na usimweshimu asiyekiongea. Kwani yeye hakuheshimu yako na ndio maana kataka ujue yake. Jua yake kwa ajiri ya samani yako na lakini usipoteze yako. Basi wote tuamie mjini basi alafu tuone maisha yatakuwaje. Matatizo yanaanza na sisi. Si selekali. Form Union!!!!!!

      Delete
  12. tunaomba majina kamili ya watu wanaofanya kazi hapo Namanga,ps,km utahitaji namba ,yangu,basi tuwasiliane ,na uongozi husika unajua? au ni hongo,?naomba majina yao hao vigogo ps,sana,hata km ni nani? hii ni aibu kwa nchi nzima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani mimi nakuunga ili tupambane nao. Forming a Union is a must for our people to get things done brother! Holding things for month is crazy!! We must wake up and stand up to protect our people's business. Otherwise we will still be living in the slaverly time era. Ndio maana uchumi wetu ni wasi wasi. Ulushwa unazidi kuabisha nchi yetu pamoja na viongozi wote. How can we form a union? Think about it, it will serve you good.

      Delete
  13. I don't think that forming the union could be the solution for our problem. The most important thing is identify problems and discuss the best way to solve them.Without understanding problems is the sign of failing to get solution for our chronic problems. If you are a good follower of the things happening in our country you can agree with me that we have few and important people who can help us to finish problems that we have but we the one we cry and blame the government every day do not understanding what is the problems. there problems we face created by ourself since we cannot identify our core problems and provide enough support to those few people who are ready to change our lives.

    ReplyDelete
  14. We have the same problem almost every where in Tanzania especialy in the airport kilimanjaro air port ,the behavior which Ifound in KIA,was so bad due toa allow other people to pass through while others be waiting ,this is the face of the nation ,if this is the case in Namanga may be wose ,we need to solve our problem no any one from out side will be there to solve our issues.

    ReplyDelete
  15. mmh hao watu wanavyouzi natamani hata niwararua kama nguo

    ReplyDelete
  16. Jaman watanzania mimi najiuliza hizi mashine za RISIT ambazo TRA wanataka wafanya biashara tunununue 800,000 kwa kweli ni kututia umaskini sisi wafabiashara wadogo kwani hazina tija kwetu ila kwao kwanini wasingeziuza bei ndogo. maana kila mfanya biashara anayeuza kama sh 40000 (Jumla sio faida) lazima awe na mashine hio. Jaman tutafika sisi kweli

    ReplyDelete
  17. Jamani watanzania tunahitaji mabadiliko.Kuna wachache ambao wanazuia mabadiliko kwa maslahi yao.Hakuna ambaye ataweza kuleta mabadiliko Tanzania isipokuwa watanzania.Angalia tu mfano jinsi matajiri wanavyokwepa kodi kwa makusudi mfano ukienda kwenye mayard makubwa ya magari,ukinunua gari unaulizwa kama unataka wakusaidie kulipa ushuru,wao hulipa tofauti kabisa na watanzania ambao kila siku wanajitafutia riziki kwa haki ambao wakiagiza kigari kimoja tu basi ushuru hulipishwa wa juu na wengi magari huwashinda na kuyaacha bandari kuishia kupigwa mnada.Je hawa matajiri kwenye mayard wanasaidiwa na kina nani TRA,serikalini,nchi huvunjwa na wananchi wenyewe.

    ReplyDelete
  18. Mh hii nchi imejaa uchakachuaji kila mahali, Hebu tuangalie hata pesa za noti, Hata nazo zimetengenezwa kwa uchakachuaji mtupu. angalia noti za sh. 500/= Ni bomu tupu, Nchi yetu tunaibiwa mno tena kwa kupindukia. Madini, Vipusa,Nyara, Wanyama wa porini. Wengine walisafirishwa waziwazi wakionekana wakapelekwa KIA kwenda kusafirishwa kwa ndege kwenda ughaibuni. Inasikitisha sana. Nadhani kuhusu our next Generation tuandike Zero. Nchi inachunwa kishenzi. And we shall be giving comments without action being taken. There is no any seriousness kwa hawa watu wa serikali. Look at the Problem of Power (nishati) Wamebaki kutudanganya danganya tu. Uchumi unazidi kwenda chini In fact we are below the red line oooow!!! Hawaangalii kabisa poor people kitu wanachojali ni namna ya kuongeza mtuno wa mifuko yao. very sorry, uzalendo umepotea kabisa. HEBU JAMANI TUWAANGALIE HAWA WATOTO WETU WATAPATA URITHI UPI? This is Pitiful.

    ReplyDelete